Email this sample to a friend

ONYESHO LA KWANZA

( Duniani Kifo anaonekana mchovu akitembea taratibu kuelekea nyumba moja nzuri, kubwa na ya kuvutia machoni.Kifo analalama peke yake,akionekana mwenye huzuni na uchovu mwingi anapoifikia nyumba ile anaingia bila kizuizi chochote moja kwa moja hadi chumba kimoja ambamo kuna mama mtu mzima anaonekana kalala, taratibu kifoanaingiza mkono mfukoni na kutoa orodha mbili ndefu.Kisha anamwamsha yule mama...)

KIFO: Ehe! Wewe ndo Amina Shabani?

AMINA: Ndio kwani wewe nani?

KIFO: Nina majina mengi ila waweza niita kifo.

AMINA: Kifo ina maana siku zangu ndo zimefika?

KIFO: Ndio na naona jina lako halipo kwenye orodha hii ya luciferi ngoja niangalie kwenye orodha ya ziraeli. Aha! Amina Shabani hili hapa kwenda peponi.

( Amina kwa taabu anamuita bintiye pamoja na kaka yake, wanapoingia Kifo anashtushwa na uzuri wa binti yake Amina. Ila wao hawamwoni ila wanapoingia tu wanahisi hali imebadilika.Anima anahema kwa tabu anajitahidi kuongea nao japo kwa shida...)

AMINA: Mwanangu Hawa mimi tena nguvu sina muda wangu umefika, naomba umsikilize mjomba wako kwani yeye ndiye mhimili pekee uliobakiwa nao hapa duniani.Zingatia mafundisho ya wakubwa zako na kuwa makini na walimwengu.

HAWA: Mama usiseme hivyo bado nakuhitaji kwani bado mengi nahitaji toka kwako.

AMINA: Usihuzunike sana mwanangu kwani hata mimi ningependa bado kuwa nanyi ila muda wangu umefika. Kaka Hamisinakuomba sana uniangalizie mwanangu mtunze kama wako kwani yeye ndo mboni ya jicho langu.

HAMISI: Usihofu dada kwani mwanao ni mwanangu pia hakuna haja ya kuniomba kutimiza wajibu wangu.Hawa ni mwanangu na atapata matunzo na malezi yanayostahili.

Previous Page Next Page Page 1 of 6